Burudani

Wimbo ‘Moyo Mashine’ umeandika historia mpya katika maisha ya muziki wangu – Benpol

Msanii wa muziki wa R&B Ben Pol amesema wimbo wake mpya ‘Moyo Mashine’ aliyouachia wiki tatu zilizopita ni wimbo ambao umebadilisha mambo mengi katika maisha yake ya muziki.
Ben Pol

Akizungumza na Bongo5 wiki hii, Ben Pol amesema wimbo ‘Moyo Mashine’ ni wimbo ambao umefanya vizuri mapema zaidi kuliko nyimbo zake zote.

“Haijawahi kutokea nyimbo yangu ikafanya vizuri hivi kwa muda mfupi,” alisema Ben Pol “Moyo Mashine sasa hivi inakaribia view laki tano YouTube ndani ya wiki mbili na nusu sawa sawa na ‘Sophia’ ambayo ina mwaka na zaidi. Kwa hiyo hii ni historia kwa sababu haikuwahi kutokea katika maisha yangu ya muziki, kwa hiyo mimi nasema asante sana mashabiki wangu, media pamoja na watu wangu ambao nimefanya nao kazi au wameshiriki kwa namna moja kwenye project hii,”

Hapi

Pia muimbaji huyo amewataka mashabiki kuendelea kusupport muziki wake huku akiwataka kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio wa albamu yake mpya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents