Michezo

WrestleMania XXX: The Undertaker alazwa hospitali, ashindwa kwa mara ya kwanza kwenye historia ya mchezo huo

Kwenye mechi ya WrestleMania XXX ya WWE, kisichowezekana kimetokea: Brock Lesnar amemshinda The Undertaker na kumaliza utemi wake wa miaka mingi.

https://www.youtube.com/watch?v=EkEK1Z8M_YI

Baada ya kuwashinda Triple H, Shawn Michaels, Edge na CM Punk kwa miaka mingi, wengi waliamini kuwa Undertaker ataendelea kutetea taji lake. Na wazo kuwa anaweza kushindwa na Brock Lesnar ndio iliyowaacha mdomo wazi kwakuwa Lesnar hakuwa akichukuliwa kama tishio.

Baada ya kushindwa mcheza mieleka huyo mkongwe alikimbizwa hospitali kutokana na kuumia vibaya na baada ya kuangaliwa kwa ukaribu aliruhusiwa jana asubuhi. Hiyo ni mara ya kwanza kwa Undertaker kushindwa katika historia ya mechi hiyo na hivyo kuwakasirisha mashabiki wengi wa mieleka walioanzisha hashtag #ThankYouTaker kumlaumu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents