Michezo

Yanga inatia huruma tu

Hali ya majeruhi kwa upande wa Klabu ya Yanga kutokana na ripoti ya mwisho ya Daktari wa timu hiyo.

Kuna uwezekano mkubwa wachezaji wafuatao wakakosekana au kuanzia benchi kwenye mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Khalid Aucho bado yupo chini ya uangalizi wa daktari hajaanza mazoezi na timu na tayari ameanza mazoezi mepesi ili kujiweka sawa.

Kibwana Shomari ameanza mazoezi binafsi licha ya kuwa nje kwa muda mrefu.

Yao Kouassi Atthoula bado anauguza kidonda chake mara baada ya kuchanika sehemu ya mguu mechi dhidi ya Azam FC.

Zouzoua Pacome bado hayupo fit kutokana na kupata enka licha ya kujumuika na timu ya Taifa ya Ivory Coast.

Zawadi Mauya huenda akapatikana kwenye mchezo ujao dhidi ya Mamelodi Sundowns siku ya Jumamosi saa 3:00 Usiku katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents