Kupitia Barau yao waliyopost @yangasc wameandika kuwa:-
“Uongozi wa Young Africans Sports Club unatoa pole kwa Uongozi wa Simba Sports Club kufuatia msiba wa shabiki wa timu hiyo aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo kwenye ajali ya gari lililobeba mashabiki waliokuwa njiani kuja Dar Es Salaam kutazama mechi za Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya Marehemu mahala pema peponi. Amen.
Pia, tunatoa pole kwa mashabiki wote waliopata majeraha kwenye ajali mbili, maeneo ya Vigwaza Pwani na Doma, Mkoani Morogoro wapone haraka waweze kurejea katika majukumu yao.
Vilevile, Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuwaomba mad-ereva na mashabiki wote wa soka wanaosafiri kutoka mikoani kuja Dar Es Salaam kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mabingwa, kuwa watulivu na kuzingatia alama za usalama wa barabarani wakati wote wa safari.
Tuwatakie safari njema wote na Mwenyezi Mungu azibariki safari zenu Amen.