Michezo

Yanga warejea kujifua dhidi ya Simba

Kikosi cha Timu ya Young Africans SC, Kimerejea Dar es Salaam kikitokea Mwanza baada ya kukusanya alama tatu katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa jana Jumapili.

Mchezo duo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Young Africans SC iliibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya wenyeji wao Singida Fountain Gate.

Baada ya kurejea Dar es Salaam, kikosi moja kwa moja kinaanza maandalizi ya kuelekea mchezo ujao wa Kariakoo Derby ndani ya Ligi Kuu NBC.

Kariakoo Derby ambayo itachezwa Jumamosi ya Wiki hit kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 11;00 Jioni Yanga itaingia Uwanjani ikiwa inaongoza Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC kwa pointu 55.

Ikumbukwe kwamba katika Kariakoo Derby ya mzunguko wa kwanza Yanga waliibuka na Ushindi wa Goli 5-1 wakiwa ugenini.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents