AfyaHabari

Zaidi ya nusu ya watu duniani watakuwa na uzito ifikapo 2035

Zaidi ya nusu ya watu duniani watakuwa na uzito wa mwili kufikia mwaka 2035 iwapo hatua hazitachukuliwa, limetahadharisha shirikisho la kupambana na unene wa mwili wa kupindukiaduniani, (World Obesity Federation ), limetahadharisha.

Watu zaidi ya bilioni nne wataathiriwa, huku viwango vikitarajiwa kuongezeka kwa kasi zaidi miongoni mwa watoto, imesema ripoti.

Nchi zenye kipato cha chini na cha kati barani Afrika na Asia zinatarajiwa kushuhudia ongezeko kubwa zaidi la watu weney uzito wa mwili wa kupindukia.

Ripoti inabashiri kuwa garama ya unene wa mwili wa kupindukia itapanda na kufikiza zaidi yad ola trilioni 4 za Kimarekani (£3.3tn) kila mwaka ifikapo 2035.

Ripoti hiyo imeelezea hasa kuongezeka kwa viwango vya uzito wa mwili wa kupindukia miongoni mwa watoto na vijana wadogo wenye umri wa kubalehe, huku viwango vyao vikitarajiwa kuongezeka mara dufu ikilinganishwa na viwango vya mwaka 2020 miongoni mwa wavulana na wasichana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents