Habari

Zitto Kabwe autaka Urais wa Tanzania

Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu amesema kuwa wao kama Chama katika miaka yao 10 kama Chama chenye usajili wa kudumu, wameweza kujijenga kitaasisi na hivyo wako tayari kuchukua mamlaka ya Nchi Zanzibar na Tanzania bara kwa kumsimamisha Kiongozi wao Mstaafu wa Chama Zitto Kabwe kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jussa ameyasema hayo jana katika sherehe za kitaifa za maadhimisho ya miaka 10 ya ACT yaliyofanyika mkoani Kigoma ambapo amebainisha kuwa Zitto anayo nafasi kubwa ya kukivusha chama hicho na kuchukua uongozi wa Nchi.

“Tunajua Mnamtaka Zitto kuwa Mbunge wenu hapa mjini kwenye uchaguzi ujao lakini sisi kama chama tunataka atuvushe kwenye nafasi ya uraisi wa Tanzania kutokana na uwezo na nafasi aliyonayo na tunaomba mtoe baraka zenu kufanikisha hilo” ———Jussa.

Kwa upaande wake kiongozi wa Chama Mstaafu,Zitto Kabwe amesema kuwa “Niko tayari na nimejianda kimaarifa na kusaikolojia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakati wowote mkinihitaji niko tayari, kuhusu ubunge hakuna shida wakina Nondo wapo na Vijana wengine wakati wowote tupo tayari kuleta mabadiliko ya ya Nchi yetu,mimi ni mstaafu napokea amri kutoka nyie Viongozi wangu”

Zitto kabwe mbali na hayo amesema miaka 10 ya kuanzishwa kwa Chama hicho inatosha kukifanya kuwa Chama kikubwa Nchini na cha Watu hivyo mpango wa miaka 10 ijayo ni mkakati wa kuhakikisha Chama kinashika dola.

Kuhusu mpango wa Chama kumtaka kugombea Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa 2025, Zitto alisema kuwa alijipanga kugombea Ubunge jimbo la Kigoma Mjini lakini Chama kinayo maamuzi na kama kitaamua hivyo basi hatokuwa na kipingamizi.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents