35% ya wanaume hupigwa Na wake zao

Spika wa Bunge, Bwana Samuel Sitta amewaacha hoi waheshimiwa wabunge alipotoa taarifa ya utafiti kuhusu wanaume wanaopigwa na wake zao huko majumbani kwao

Spika wa Bunge


 


Spika wa Bunge, Bwana Samuel Sitta amewaacha hoi waheshimiwa wabunge alipotoa taarifa ya utafiti kuhusu wanaume wanaopigwa na wake zao huko majumbani kwao.


 


Ali hiyo ilijitokeza huko Bungeni mara baada ya kumaliza kipindi cha maswali na majibu ambapo Spika alieleza kuwa ana ujumbe kutoka kwa mmoja wa wabunge ambaye amemuomba kurudia taarifa yake kuhusiana na utafiti huo ambao umeonekana ni kivutio kwa wabunge.


 


“Nimepata ujumbe hapa tena kutoka kwa mheshimiwa mwanamke ambaye ananiomba nirudie kutamka kuhusiana na utafiti wangu huu” alisema Spika.


 


Spika alisema utafiti unaonyesha asilimia 35 ya wanaume wanapigwa na wake zao ingawa hawasemi kutokana na kuona aibu na kufedheheka.


 


Alisisitiza kuwa asilimia hiyo inajumuisha pia waheshimiwa wabunge wanaume ambao hukandamizwa makonde huko majumbani kwao na wake zao sema wakiwa kwenye halaiki hujitutumua na kujifanya mashujaa kumbe wakirudi makwao cha moto wanakipata.


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents