Habari

Abdul Nondo anyimwa dhamana Iringa

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo amesomewa mashtaka mawili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa.

Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la Mwananchi umesema, makosa hayo ambayo Nondo ameshtakiwa ni pamoja na kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni March 7 ya mwaka huu kuwa yupo maisha yake yapo hatarini akiwa katika eneo la Ubungo na kuzisambaza kwenye mtandao wa Whatsapp.

Kosa la pili limetajwa kuwa ni kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma Mafinga wakati alipokuwa akitoa taarifa katika kituo cha polisi mjini humo kwa kusema kuwa alitekwa na watu wasiojulikana.

Hata hivyo Nondo ameshindwa kupatiwa dhamana kutokana na Hakimu John Mpitanjia kudai kuwa wanalinda usalama wake kutokana na maisha yake kuwa hatarini.

Hakimu Mpitanjia ameomba muda wa kuvisoma vizuri vifungu vya sheria ili kujihakikishia kama mtuhumiwa huyo anaweza kupatiwa dhamana mpaka ifikapo March 26 ya mwaka huu.

Chanzo Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents