Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Achana na muziki; Bill Nass ajibu kuhusu kuajiriwa

Msanii Bill Nass amefunguka iwapo ana mpango wa kutaka kuajiriwa baada ya kuhitimu masomo yake mwaka jana.

Bill Nass ameeleza kuwa anahitaji kufanya kazi ila anahitaji sehemu ambayo itamtambua kama msanii ili awe huru kufanya muziki wake.

“Bado kuna vitu nilikuwa natamani sana nivifanye mtaani halafu nione kwa sababu ajira ni comitment nyingine. Natamani kufanya lakini kwenye taasisi au kampuni itakayotambua huyu ni Bill Nass,” amesema.

“Kwa sababu wao wanaweka fedha zao ila wanatakiwa watambue huyo mtu kuna kitu kingine anaweza kukifanya. Nataka nipate hiyo sehemu, nisiharibu kazi yao lakini nao wasione kama nawazingua,” Bill Nass ameiambia Bongo5.

Bill Nass ni msomi wa ngazi ya shahada ambapo amechukulia manunuzi na ugavi. Kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake Tangi Ubavu na kolabo kadhaa alizofanya na wasanii kama Mwasiti na Rosa Ree.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW