Burudani

Afande Sele aonyesha picha za mtoto wake wa Mwanza aliyempatia jina la producer P Funk ‘Majani’

Msanii wa muziki wa hip hop, Afande Sele Jumamosi hii ametupia picha mtandaoni ya mtoto wake ambaye hakuwahi kumuonyesha hadharani.

Rapa huyo mkongwe amesema mtoto huyo amempatia jina la Majani kutoa heshima kwa producer mkongwe wa muziki wa BongoFleva P Funk Majani.

“Katika maisha yangu ya muziki niliweza kufika Mwanza mara nyingi zaid kuliko mkoa wowote ndani ya nchi yetu…lkn ukiniuliza ni kitu gani ninachojivunia kutoka Mz nje ya kufanya show za mziki na kukubalika kupita kiasi?. Jibu langu ni rahisi tu kwamba nilibahatika kumpata huyu mvulana mdogo mwenye miaka kumi sasa hivi ambae tangu akiwa tumboni mwa mama yake nilimpa jina la Majani kama heshima kwa producer wangu wa kihistoria aliyechangia kiasi kikubwa kufanya mimi niwe mwanamuziki…Huyu ndio kaka pekee wa kina Tundajema na Ahsantesanaa….yeye ndio mrithi wangu wa baadae….Majani Selemani Msindi,” aliandika Afande Selle.

Afande yupo mkoani Mwanza kwasasa kwaajili ya shughuli zake za muziki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents