Michezo

Picha: Marcus Rashford aibeba United mbele ya Bournemouth

Klabu ya Manchester United imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 1 mbele ya Bournemouth kwenye mchezo wa ligi ya Uingereza.

United imepata ushindi huo kupitia bao la dakika zanyongeza (90+2) kabla mpira huo kumalizika kupitia kwa nyota wake Marcus Rashford.

Katika dakika 90 za mtanange huo mabao yalikuwa 1 – 1, kwaupande wa Bournemouth goli likifungwa na Wilson dakika (11) kisha United ikasawazisha kupitia Martial (35).

Kwa matokeo hayo Man United inakuwa na jumla ya pointi 20 kwenye michezo 11 iliyocheza na kushika nafasi ya saba wakati vinara wa ligi Man City wakiwa na alama 26 ambazo ni sawa na Liverpool.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents