Habari

Afisa wa juu wa polisi Dar ahukumiwa kunyongwa, Zombe aachiwa

Mahakama ya Rufani imemhukumu kunyongwa hadi kufa, aliyekuwa Mkuu wa upelelezi wilaya ya Kinondoni, (SP) Christopher Bageni baada ya kumtia hatiani kwa kosa la mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro.

mahakama_

Wakati huo huo mahakama hiyo imewaachia huru maafisa wengine watatu akiwemo aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe, Ahmed Makelle na Rajabu Bakari.

Ni muda mrefu kumekuwa na mvutano mkubwa wa kesi hiyo ambayo ilikuwa ikiwatuhumu maafisa hao wa polisi kutekeleza mauaji ya wafanyabiashara hao wa madini kwa makusudi Januari 14, 2006 ambao walifahamika kwa majina ya Sabinus Chigumbi, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na aliyekuwa dereva teksi, Juma Ndugu.

Awali DPP aliiomba mahakama imtie hatiani Zombe kwa kosa la kuwalinda wahalifu, ambao adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka saba jela lakini hakimu alishindwa kufanya hivyo kutokana na kutoridhishwa na ushahidi uliyokuwepo wa kumtia mtuhumiwa huyo hatiani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents