Habari

Afrika Kusini: Jaji aliyetoa matamshi ya kibaguzi ajiuzulu

Jaji mwenye asili ya kizungu nchini Afrika Kusini, amejiuzulu baada ya kutoa matamshi ya kibaguzi mwaka jana, katika mitandao ya kijamii akisema kuwa matukio ya ubakaji ni utamaduni wa watu weusi.

Jaji huyo wa Mahama Kuu, Mabel Jansen, alikuwa katika mapumziko akisubiri upelelezi wa mahakama kufanyika juu ya sakata hilo. Matamshi hayo yalisemwa na rafiki yake ambaye hakutajwa jina.

Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi zenye asilimia kubwa ya matukio ya ubakaji duniani.

Na Emmy Mwaipopo

Chanzo: BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents