Habari

Mfanyabiashara maarufu ahukumiwa jela miaka 25 kwa kusafirisha meno ya tembo

Mahakama ya hakimu mkazi Tanga imemhukumu kwenda jela miaka 25 na faini ya shilingi bilioni 4 mfanya biashara Michael Kijangwa baada ya kupatikana na kosa la kusafirisha meno ya tembo yenye uzito wa tani elfu 5.

Hukumu hiyo imetolewa mbele ya hakimu mkazi mfawidhi Clinsesia Kisango baada ya ushahidi wa upande wa jamhuri kumkuta na hatia ya kusafirisha meno ya tembo nje ya nchi kinyume cha sheria. Akisoma hukumu hiyo hakimu mfawidhi Clinsesia Kisango, Kijangwa alitiwa hatiani kwa makosa yaliyokuwa yakimkabili ikiwemo la kukutwa na nyara za serikali kula njama kusafirisha pamoja na kupakia mizigo bila ya ukaguzi na mamlaka husika.

Ambapo kwa upande wa kosa la kupakia mzigo bila ya ukaguzi adhabu yake ni faini ya shilingi 50,000 na kutumikia kifungo cha miaka 5 vyote hivyo vinakwenda kwa pamoja. Katika utetezi wake Kijangwa alisema ameridhishwa na mwenendo wa kesi hiyo inavyoendeshwa na hana pingamizi na hukumu ambayo mahakama hiyo imetoa dhidi yake.

Vile vile aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kutokana na kuwa mke wake ni mgonjwa wa kiharusi na ndiye anaemtegemea hivyo kufungwa kwake kunaweza kusababisha madhara mengi kwa mkewe huyo. Hata hivyo utetezi huo ulipingwa na hakimu wa serikali huku akitaka adhabu hiyo itolewe kutokana na kosa alilolifanya Kijangwa ili iwe fundisho kwa wengine.

BY: EMMY MWAIPOPO

CHANZO: TBC1

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents