Michezo

Wenger: Nilikuwa nahofia sana kumchezesha Sanchez kama mshambuliaji wa kati

kocha Arsene Wenger amesema kuwa mwanzoni alipatwa na hofu kwamba alikuwa anafanya makosa kumchezesha Alexis Sanchez kwenye nafasi ya mchambuliaji wa kati awapo uwanjani.

Wenger mwaka 2014 alimchezesha kwa mara ya kwanza katika nafasi hiyo kwenye mechi dhidi ya Everton na kumtoa wakati wa mapumziko baada ya kujiona alikuwa amekosea kufanya hivyo.

Pamoja nahayo yote kutokea Wenger amejipatia matunda ya uamuzi wake na sasa anaamini kwamba Sanchez ndiye mrithi wa staa wa zamani wa timu hiyo, Thiery Henry.

Kwa hivi sasa Sanchez amekuwa ni mfungaji tegemeo wa klabu ya Arsenal na anafanana na Henry kwa uwezo wake wa kupachika mabao, na kutoa pasi, chenga na mbio awapo uwanjani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents