Habari

Ajinyonga kwa kutengwa na familia

MKAZI wa Kimara jijini Dar es Salaam, Gerald Mwashitata, amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani kwa madai ya kutengwa na familia yake baada ya kugundulika anaishi na virusi vya Ukimwi.

Mwandishi Wa Habari Leo

 

 

 

MKAZI wa Kimara jijini Dar es Salaam, Gerald Mwashitata, amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani kwa madai ya kutengwa na familia yake baada ya kugundulika anaishi na virusi vya Ukimwi.

 

 

 

Mwashitata (48) alikutwa amejinyonga chumbani kwake juzi majira ya saa 5 asubuhi, na aliacha ujumbe unaosema ‘Pole sana kaka Arthur, nimejinyonga kutokana na familia kunitenga’.

 

 

 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Jamal Rwambow, alisema Mwashitata alikuwa akiumwa tangu mwaka juzi baada ya mkewe kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo wa Ukimwi.

 

 

 

Maiti imehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala. Katika tukio jingine, mfanyakazi wa duka la kuuza vipuri vya magari la Specializedeng (T) Ltd, Gottipati Sivarama (54), amejeruhiwa kwa risasi katika shavu la kushoto baada ya majambazi kuvamia duka hilo lililopo barabara ya Nyerere.

 

 

 

Alitibiwa katika Hospitali ya Aga Khan na kuruhusiwa. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alisema majambazi hao watatu waliokuwa na bunduki walivamia duka hilo juzi saa 2:30 asubuhi na kuwaweka chini ya ulinzi wafanyakazi wote na walipora Sh milioni mbili za mauzo na simu tano za mkononi ambazo ni za wateja.

 

 

 

Wakati huohuo, dereva teksi Athumani Kadini (21), ameibiwa gari yake na watu wasiojulikana ambao walikodi teksi hiyo. Kamanda Rwambow akielezea tukio hilo lililotokea juzi saa 5 usiku, alisema Kadini alikodiwa teksi yake na mtu mmoja kutoka eneo karibu na Mahakama ya Kinondoni ili ampeleke Kwa Manyanya na walipofika njiani alimuomba wasimame wawachukue wenzake ambapo dereva huyo alipotii, alivamiwa na watu hao waliomtoa nje ya gari na kukimbia nalo.

 

 

 

Source: Habari Leo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents