Habari

Ajira popote

Mtoto_dili_Face

Jana nikiwa Temeke kwenye uchukuaji wa video ya mwanamuziki Feroozi, nikajionea mambo mengine ambayo yalinifanya niyachunguze kwa muda bila ya kupata jibu. Huyu mtoto yeye ameingia kwenye ajira ya kuokota makopo wakati wenzake wakiangaika na kucheza muziki. Nilimshangaa sana alivyokuwa bize kuokota kila kopo la maji, ambalo mtu anadondosha,  ndipo nikajiuliza hivi kweli tutafika kama mtoto mdogo kama huyu hata dalasa la kwanza hajaanza na kama ameanza hata kusoma hajui, lakini kashaanza kuokota makopo…

mtoto_dili_la_kopo

Hapa alikuwa akiweka kopo kwenye mfuko, huku akiangaza kutafuta kopo lingine yeye hakuwa na habari hata kidogo ya muziki uliokuwa ukiendelea. nilipomuuliza unayapeleka wapi, alinijibu kwa kifupi ‘Naenda kuuza’, kisha akanipotezea.

mtoto_dili_lingine

Aliendelea kusaka makopo ya maji, kila sehemu….

mtoto_dili_akitulia

Kuna kipindi nilimuona amechoka sana na kupumzika na wenzake , lakini hazikupita dakika nyingi akainuka na  kuendelea kutafuta makopo… NI MIAKA 50 TU   YA UHURU,  BADO 50 NYINGINE TUFIKISHE 100….

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents