Burudani

Albino Fulani: Atoa Single mpya akimshirikisha Pipi

Albino Fulani atoa track mpya ambayo amemshirikisha Pipi msanii mahiri wa kizazi kipya inayoenda kwa jina la USIHOFU (Niko na wewe) imeanza kufanya vizuri maredioni toka ilivyozinduliwa kwenye XXL ya Clouds FM siku chache zilizopita. Albino Fulani (AF) ambaye kwa sasa yuko marekani kikazi, akiongea na ofisi zetu za bongo5 leo alisema hii ni historia ya kweli aliyoizungumzia kwa uchacheĀ  kwenye mziki kwamba ndugu wa msichana aliyempenda walijitahidi kufanya fitna ili wasiwe pamoja kisa ye ni albino na kuwa huu ni mziki wake wa kwanza husiana na mambo ya kimapenzi.

Fulani yuko mbioni kutoa album ambayo mapato yake ataelekezea katika kusaidia Maalbino wenzake kama mchango na chachu ya kuamsha albino wenzake kuwa wasikate tamaa na maisha kwani nafasi bado wanayo kama alivyowaambia kwenye track yake iliyopita ambayo alimshirikisha MwanaFa, Belle9, & Sugu.

Hivi karibuni Albino Fulani alitoa misaada ya lotions za kinga za jua kwa maalbino wenzake Tanzania kupitia shirika lisilo la kiserikari la Afrobino.org katika jitihada zake za kupambana na Cancer ya ngozi.

Bofya hapa kusikiliza ngoma “Usihofu, Nikoa na Wewe”

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents