Burudani

Ali Kiba asepa zake Naija

Mwandishi wa Bongo5 alikutana na Ali Kiba alfajiri ya Ijumaa akiwa anaelekea zake uwanja wa ndege kupanda ndege ya Kenya Airways na alipoulizwa kwa upole tu na tabasamu ndefu akajibu anakwenda Lagos nchini Nigeria kwa ajili ya uzinduzi wa African super group One8.

Ali kiba ameendelea kutamba baada ya kuwa msanii wa kitanzania ambaye hakai bongo zaidi ya wiki tatu kabla hajasafiri kupiga shoo. Muimbaji huyo mwenye masongi yenye hisia kali ameonekana kung’ara zaidi kwa sasa baada ya juzi tu kutoka Chicago nchini Marekani kurekodi na msanii R. Kelly pamoja na wasanii wengine saba wa kiafrika (Amani, Fally Ipupa, Tuface, JK, Movaizhaleine, Navio na 4X4) katika project ya Muziki, iendayo kwa jina la Hands Across the World.

Ali Kiba mpaka sasa ameshazunguka mabara ya Afrika,Ulaya, Marekani na Australia huku akisubiri mwaliko wa kwenda bara hindi kukamilisha mzunguko wa mabara yote matano duniani.

Bongo5 inakuahidi kukupa maelezo zaidi ya safari hiyo ya Ali Kiba Nigeria. Stay tuned

Pata official video relase ya wimbo “Hands Across the World” hapa chini:

{hwdvs-player}id=1259|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents