Burudani

Alichosema Flaviana Matata baada ya kukutana na Beyonce na Jay Z

Mwanamitindo wa kimataifa kutoka Bongo, Flaviana Matata ameeleza mambo machache kuhusu tukio la kukutana na Jay Z na Beyonce.

Weekend iliyopita Flaviana kupitia ukurasa wake wa twitter aliweka video akiwa na mastaa hao wa dunia. Akizungumza na XXL ya Clouds Fm Flaviana amesema walikutana katika maonyesho ya magari ya zamani ambayo yalikuwa ya kifahari lakini hawakuzungumza sana.

“Perfect nilikuwa kwenye event ya mambo ya magari, Hamptons nikakutana nao, Jay nimekutana naye mara nyingi sana, Beyonce this is first time I think but people get excited kwa sababu it had never meet to the internet,” amesema Flaviana.

“Sijawahi kuwa na video picha lakini those people we meet husalimii, kila mtu anaendelea na hamsini zake, pale tulikuwa tunasalimiana, hongea kwa watoto and then nikamsalimia Jay nikaenda zangu,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents