Burudani

Alikiba anena Barakah kuondoka RockStar4000, ‘muache dunia imfunze’

Msanii Alikiba amezungumzia kitendo cha Barakah The Prince kuondoka RockStar4000 na kusema wameamua kumuacha dunia imfunze kwanza.

Muimbaji huyo ambaye ni miongoni mwa wamiliki wa RockStar4000, ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa mkataba wa menejiment hiyo na Barakah ulikuwa wa miaka mitatu ila kila baada ya mwaka mmoja huwa wanapitia upya.

Ameendelea kusema iwapo muhusika hakuweza kuiletea menejineti faida anaondolewa na ndicho kilichotokea kwa Barakah The Prince.

“Tunaangalia vipi unatuletea mpunga, kwa hiyo kama hujatuleta mpunga tunazima taa vile vile,” amesema.

Ameongeza kuwa alijuana na Barakah baada ya kuwa naye RockStar4000 lakini hakufurahishwa na vitu ambavyo alikuwa akivifanya, mwanzoni alikuwa akiona kama utoto lakini akagundua si utoto tena.

“Nimeona amenikosea heshima kwa hiyo nikaona haina haja, na mimi nikiwa kama mtu mzima sitakiwi kugombana na mtu mdogo. Unatakiwa umuache dunia imfunze kidogo au kama kuna kitu amefanya au amelishwa sumu basi akapewe dawa itoke,” amesema Alikiba.

Hata hivyo Alikiba amekiri kuwa Barakah ni msanii mzuri na mwenye kipaji ndio sababu ya kuwepo RockStar4000.

Alikiba kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Seduce Me’ aliotoka August 25, 2017 na kuweka rekodi ya kufikisha views Milioni 2 ndani ya siku tatu katika mtandao ya YouTube.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents