Michezo

Ally Mayay atia neno kwa viongozi wapya wa TFF

Baada ya uchaguzi mkuu wa TFF kumalizika jana mjini Dodoma na kupata viongozi wapya watakaohudumu kwa miaka minne, aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais, Ally Mayay amedai uchaguzi ulikuwa ni wa huru na haki kwa wagombea wote huku akiwapongeza washindi.

Ally Mayay

Ally Mayay ambaye kura zake hazikutosha amesema hataacha kulitumikia soka la Tanzania kwani maisha yake ni mpira tosha na ataendelea kuwaunga mkono viongozi wapya wa TFF.

“Sisi ndio waasisi wa mpira wa miguu na dhana na fair play unafungwa magoli 9-0 na unaondoka na kwenda kumuunga mkono aliyekufunga mnakaa pamoja na kunywa wine…kwani kabla ya uchaguzi tulikuwa tunafanya kazi ya mpira na tutaendelea kufanya kazi ya mpira na viongozi waliochaguliwa”,amesema Ally Mayay alipoulizwa kama ataendelea kuwaunga mkono viongozi teule wa TFF huku akisifia mchakato wa uchaguzi huo ulivyokuwa wa haki.

“Tunashukuru sana wajumbe kwa uchaguzi na tumemaliza vizuri kamati imesimamia uchaguzi ulikuwa huru na haki, mambo yamekwenda vizuri watu wamezungumza content, Uchaguzi ulikuwa fair na tunaunga mkono”,amesema Ally Mayay mbele ya waandishi wa habari jana baada ya uchaguzi kumalizika.

SOMA ZAIDI: Wallace Karia rais mpya TFF

Ally Mayay ni moja ya wagombea wa Urais TFF waliokuwa wamepewa kipaumbele cha kuchukua nafasi hiyo ya heshima lakini kura hazikutosha kukalia kiti hicho na badala yake nafasi hiyo imechukuliwa na Wallace Karia.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents