Habari

Amani (Kenya) awaelimisha vijana kutokana changamoto za maisha alizopitia

Mwanamuziki mrembo wa nchini Kenya, Cecilia Wairimu aka Amani ambaye kwa sasa anatamba na kazi yake mpya ‘Kiboko Changu’ amesema katika kipindi alichokuwa kimya kimuziki amekuwa akijishughulisha zaidi na shughuli za kijamii.

amani281211 (1)

Amesema alikuwa akifanya shughuli za hisani kwa vijana kuwashauri na kuwapa mawazo chanya juu ya maisha.

Ameweka wazi kuwa alikuwa akifanya kazi hiyo hasa kutokana na historia yake alipokuwa madogo. Amesema awali alikuwa hajikubali kutokana na kuwa mnene kupita kiasi na kuonewa na wengine, kitu kilichokuwa kinamuathiri kisaikolojia lakini baada kufanikiwa aliishinda.

Amesema fani ya kuimba ndio iliyomsaidia kusimama na kujiona kuwa yeye ni muhimu na ana nafasi katika jamii, kitu ambacho kimemsaidia kufika hapo alipo.

Source: EATV

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents