Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Amber Rose adai kunyanyaswa na Kanye West

Mwanamitindo kutoka Marekani, Amber Rose ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu kuzungumzia mahusiano yake na rapper Kanye West amefunguka kwa mara ya kwanza mambo aliyofanyiwa na rapper huyo wakati wa mahaba yao.

Akiongea katika kipindi cha Complex, mrembo huyo ameeleza kuwa wakati wa mahusiano yake na rapper Kanye alikuwa akionewa  na kunyimwa uhuru na mwanaume huyo, pia alibainisha  kuishi na mtu kama huyo ni kazi sana,

Hata hivyo mrembo huyo alikataa kuongela juu ya Boss Yeezy kuwa na matatizo ya akili. Wawili hao kwa sasa wamekuwa kama maadui kwani Amber alidai kukasirishwa na Kanye kwa kauli yake aliyiotoa kwa mtoto wake Sebastian.

Amber kwa  sasa anadate na rapper 21 Savage, huku  Kanye kamuao mrembo  Kim Kardashian na wana watoto wawili huku wakitarajia motto wa tatu kutoka kwa mwanamke aliyepoandikizwa mbegu.

Na Laila Sued

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW