Habari

Anglikana Dodoma wazidi kufukuzana

Askofu Godfrey Mhogolo wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dodoma, amewafukuza kazi viongozi wake wasaidizi, kwa madai kuwa wanamsaliti.

Na Mary Edward, PST Dodoma



Askofu Godfrey Mhogolo wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dodoma, amewafukuza kazi viongozi wake wasaidizi, kwa madai kuwa wanamsaliti.


Wanaotimuliwa ni wale wanaoendeleza misimamo yao ya kumpinga, kwa madai yake ya kuendelea kupokea fedha kutoka katika kanisa linaloshabikia ushoga.


Askofu Mhogolo kwa sasa ametengwa na parishi zake 132 kati ya 200 kwa madai ya kutetea ushoga.


Tayari, Askofu huyo amemfukuza kazi Mwenyekiti wake wa Walei, Bw. Elia Ngambusu, kwa madai kuwa, amemsaliti kwa kuungana na Askofu Msaidizi Ainea Kusenha, aliyemsimamisha kazi, kwa madai ya kupinga maamuzi yake anayotoa.


Moja ya maamuzi ambayo yanadaiwa kupingwa na Askofu Kusehna na Mwenyekiti huyo ni msimamo wake (Mhogolo) wa kushabikia ushoga, kuruhusu waumini kutumia kondomu na uongozi wake wa kibabe na kutopenda kushauriwa.


Katika barua aliyoandikiwa na Askofu Mhogolo ya kusimamishwa kazi na ambayo PST ilipata nakala yake, Mwenyekiti huyo wa Walei alisema, sababu nyingine iliyomfanya afukuzwe ni pamoja na kuingia na katiba kwenye vikao na kuisambaza, ikiwa ni pamoja na kupinga maamuzi ya halmashauri kuu.


`Ni kweli mimi naingia na katiba katika vikao kwa kuwa sikubaliani na wenzangu juu ya uamuzi wa Askofu Mhogolo kumfukuza kazi Askofu Msaidizi… kwa sababu halmashauri ilimwagiza Mhogolo achukue hatua kwa mujibu wa katiba…kitendo ambacho hakukifuata,` alisema Ngambusu.


Akizungumza na PST katika Parishi ya Chang`ombe, alikokuwa akitoa huduma ya kiroho, Askofu Kusehna alisema, kusimamishwa kwake hakutambuliki, kwa kuwa hakujafuata katiba na pia kwa mujibu wa katiba, Askofu Mhogolo hana mamlaka ya kumsimamisha kazi, isipokuwa mkutano wa Sinodi.


`Kwa hali hiyo ndiyo maana nipo hapa leo naendelea kutoa huduma ya kiroho kwa waumini wangu�na nitaendelea kupingana na Askofu Mhogolo kutokana na kitendo chake cha kukiuka katiba, taratibu na sheria zilizowekwa na kanisa katika utoaji wa huduma`alisisitiza Kusehna.


Askofu kusehna ambaye aliteuliwa na waumini wake hivi karibuni kuwa askofu wao baada ya kumkataa Mhogolo kwa madai kuwa anashabikia ushoga, amekuwa na mialiko mingi kutoka katika parishi mbali mbali wakimtaka kwenda kutoa huduma za kiroho katika maparishi hayo.


Akiwa katika parishi ya Channg�ombe ambayo ni parishi ya kwanza kumwandikia barua Askofu Mhogolo ya kumkataza kutoa huduma ya kiroho katika klanisa hilo, Askofu Kusenha amepokelewa kwa shangwe za ngoma na vigelegele.


Askofu kusehna alisema amefarijika kuona waumini wengi wanaungana naye katika kupinga kwa nguvu zote vitendo vya ushoga ili kujenga imani iliyo thabiti kwa vizazi vijavyo katika kumtumikia Mungu.


Naye Canon Elia Nhukuwala akizungumza na waumini katika ibada hiyo, alisema dhambi ya ushoga ni dhambi ya makusudi hivyo yeyote anayebainika kuishabikia na kutenda hatakiwi kusamehewa.


Alisema kwa maana hiyo hata kitabu kitakatibu cha Mungu kimeelezea kitendo hicho kichafu cha ushoga kuwa ni dhambi isiyosamehewa na kwamba mtu yeyote atakayebainika kuitenda, adhabu yake ni kutengwa.


Askofu Mhogolo ambaye anaungwa mkono na parishi 68 kati ya parishi 200, amekuwa na wakati mgumu wa utoaji huduma ya kiroho, baada ya waumini wake kumfukuza katika baadhi ya parishi wakimtaka akanushe kauli yake ya kuunga mkono vitendo vya ushoga na usagaji.


Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents