Michezo

Arjen Robben akiri kudanganya kujiangusha ili timu yake ipewe penalti

Mshambulizi wa Uholanzi, Arjen Robben amekiri kuwa katika mechi yao jana dhidi ya Mexico alidanganya kwa kujiangusha ili timu yake ipate penalti.

k (2)

Robben aliambia runinga ya Uholanzi, NOS kuwa alidanganya kwa kujiangusha. “Nataka kwanza kuwaomba radhi mashabiki wangu kwa kudanganya na kujiangusha ukweli haikufaa,” Alisema Robben. Kocha wa Mexico Miguel Herrera amemkashifu refarii wa mechi yao na Uholanzi Pedro Proenca kwa kuipendelea Uholanzi. Herrera amesema kuwa Penalti hiyo dakika tatu kabla ya kukamilika kwa mechi hiyo haikufaa”hiyo ni njama ya FIFA kuiondoa Mexico kwenye kinyang’anyiro hicho .

Uholanzi walipigana wakiwa nyuma kwa goli moja mpaka alivyosawazisha katika dakika za mwisho kupitia Wesley Sneijder na dakika 3 kabla ya mpira kumalizika Jan-Klaas Huntelaar wa Uholanzi alifunga goli la ushindi kwa mkwaju wa penalty na kuibuka na mshindi kwa mabao 2-1. Mexico ilikuwa imeongoza hadi dakika ya 88 ya kipindi cha pili kabla Wesley Sneijder kuisawazishia Uholanzi kabla ya Huntelaar kufunga penalti iliyozua ubishi mkubwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents