Michezo

AS Monaco yatwaa Ubingwa baada ya miaka 17

Klabu ya AS Monaco ya nchini ufaransa hapo jana wametwaa taji la ligi hiyo kwa mara ya kwanza, tangu wafanye hivyo miaka 17 iliyopita, ushindi wao wa magoli 2 kwa 0 walioupata nyumbani dhidi ya klabu ya Saint-Etienne uliwatosha kabisa kutangaza ubingwa msimu huu.

Kwa ushindi huo umewafanya wababe wa ligi hiyo ya Ufaransa klabu ya Paris St-Germain kuondolewa katika kinyang’anyiro hicho msimu huu kwa kuzidiwa alama tatu dhidi ya vinara hao na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Klabu hiyo imeonekana kuwa na wachezaji vijana na hivyo mafanikio yao yanakwenda sawia na umri wao, kwani mara ya mwisho Monaco kushinda taji hilo la ligi walikuwepo wachezaji wa kifaransa kama Fabien Barthez, David Trezeguet pamoja na Willy Sagnol.

Mafanikio ya AS Monaco msimu huu ni makubwa mnoo ambayo yamechangiwa na wachezaji kama Falcao raia wa Colombia na kijana mdogo wa kifaransa, Mbappe.

Falcao, mwenye umri wa miaka 31, hakuwa na msimu mzuri alipokuwa katika klabu ya Manchester United pamoja na Chelsea, ambapo alishinda magoli matano tu katika michezo yake 36 aliyoingia uwanjani.

Nahodha huyo wa Monaco sasa ameshinda jumla ya magoli 24 na kuchangia pasi 4 zilizo zalisha magoli.

Mbappe, ambaye ameonyesha makali yake zaidi katika michuano ya klabu bingwa, ameshinda jumla ya magoli 15 msimu huu. Mchezaji huyo anapigiwa chapuo kuwania tuzo ya mwaka ya mchezaji bora mwenye umri mdogo zaidi.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents