Burudani

Aslay akubali yaishe kwa Beka wa Yamoto Band

Baada ya kauli ya Beka Flavour kuwa hatomvumilia Aslay iwapo atatoa ngoma nyingine, Aslay amesema hilo halina shida.

Aslay ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Baby’, amesema hafikirii kuwa kitendo cha Beka Flavour kuhairisha kutoa ngoma ili zisigongane na yake ni kumuhofia kwani ni msanii mzuri mwenye muziki mzuri.

“Mfano mdogo Libebe imepita na hata angeamua kutoa ngoma na mimi zingekutana huku mjini na kila shabiki angependa ngoma kwa wakati wake,” Aslay ameiambia E-Newz ya EATV.

Muimbaji huyo ameongeza kuwa kitendo cha Beka kuhairisha kutoa ngoma kinaweza kuwa sawa lakini angependa kumuona akitoa kazi nyingi zaidi kwa kuwa ni ndugu yake.

Alipoulizwa kuhusu kauli ya Beka kuwa yeye ni mdogo kwake kimuziki alijibu, “mimi ni mdogo kweli, hivyo tu”.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents