Burudani

Aslay azungumzia utofauti aliouona baada ya kufanya video na Godfather

Wiki iliyopita Yamoto Band walishoot video ya wimbo wa ‘Cheza Kimadoido’ na muongozaji wa video wa Afrika Kusini, Godfather.

IMG_9455
Yamoto Band wakiwa kwenye kikao na Godfather kabla ya kufanya video ya Cheza Kimadoido

Aslay ameiambia Bongo5 kuwa walijikuta wanamuogopa muongozaji huyo ambaye anasifika barani Afrika kwa video zake bora.

“Unajua kufanya naye kazi kwa mara ya kwanza tumejikuta tuna uoga lakini mwisho wa siku tuliweza kupangana nao na kupata kitu kizuri,” amesema Aslay.

“Mazingira mazuri halafu wenzetu wapo serious. Unaweza kukuta kama Godfather ana watu wake kama 20 nyuma, yaani wote wanasimamia kazi. Mimi nasema mashabiki wasubiri, nisije nikaongea sana kwa kukiona kizuri halafu watu wakaja kukiona kibaya.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents