Burudani

Madam Rita aelezea msimu mpya wa Bongo Star Search (Exclusive Video)

Shindano la Bongo Star Search linarejea tena mwaka huu baada ya kuwa kimya kwa mwaka mmoja.

Shindano hilo ambalo kwa miaka mingi lilikuwa likidhaminiwa na kampuni ya Zantel, limepata mdhamini mpya, Salama Condoms.

Mkurugenzi Mkuu wa Benchmark Productions ambao ni waandaji wa shindano hilo, Rita Paulsen, ameiambia Bongo5 kuwa ukimya wa mwaka mmoja ulitokana na nia yao ya kuibrand upya show yao baada ya kutoka kuwa Epiq Bongo Star Search.

“Ule ukimya ilikuwa kidogo to put the show down, debrand, tukija tunakuja Bongo Star Search na hiyo imesaidia kupata sponsor mwingine,” amesema Madam Rita.

Rita amesema shindano la mwaka huu limekuja na mapya mengi ikiwa ni pamoja na kuongeza mitindo kwenye muziki. Amesema hiyo imetokana na ukweli kuwa kiwanda cha muziki kinawahitaji wasanii kuvaa vizuri ili kulinda hadhi yao.

“Sasa hivi dunia inavyokwenda kila mtu wants to look good kwahiyo tumeona kwamba tuunganike na wabunifu wa mitindo, tunawapa na wao platform na pale na wenyewe wanaweza kufaidika. Kwahiyo this time ni BSS kukuza vipaji na kutoa platform kwa wanamitindo na naamini na wao watafaidika kwa ukubwa wa show.”

Jipya jingine ni shindano hilo kuunganika na Tip Top Connection kusimamia wasanii watakaotoka kwenye show hiyo. “Kwahiyo wao wataangalia kuanzia Top 10 na watachagua watu watakaowasimamia.”

Hata hivyo mwaka huu shindano hilo litazunguka kwenye mikoa minne tu, Mwanza, Mbeya, Arusha na Dar.

Madam Rita amesema wameamua kufanya hivyo kwakuwa wamegundua kuwa washiriki wengi wa mikoani wamekuwa wakizunguka katika mikoa hiyo kama wakishindwa kupita katika mikoa wanayotoka.

“Kwahiyo tumeamua kufanya kikanda, yes kama unataka kufanikiwa inabidi ujitume, safiri, nenda hapo nenda pale. Hakuna vitu vizuri ambavyo vinakuja kirahisi,” amesisitiza Madam.

Rita amesema usaili utaanzia Mwanza kuanzia July 3 – 5 kwenye hoteli ya Lakairo, kisha Arusha, Mbeya na Dar es Salaam.

Kwa upande wa zawadi amesema itakuwa kubwa zaidi mwaka huu na wataitaja siku zijazo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents