Burudani

Harmonize: Najuta kusaidiwa na Diamond

‘Staa wa Bongo Fleva Harmonize ni kama ameonyesha kuchoshwa na kauli ambayo Diamond Platnumz anapenda kuisema mara kwa mara kuwa yeye ndiyo aliyemtoa katika Muziki.

Harmonize ameyasema hayo kupitia (Instastory) yake ambapo amepost moja ya story iliyoripotiwa na chombo cha habari cha mtandaoni nchini kikieleza namna Diamond alivyomtoa msanii huyo.

“Nilimtoa!!, Nilimtoa!!, Nilimtoa!!, Nilimtoa!!, ndio ni kweli asante ila inachosha na nakaribia kujuta, Ameandika Harmonize.

Harmonize aliwahi kuwa mmoja wa zao la muziki kutoka lebo ya WCB Wasafi chini ya usimamizi wa msanii Diamond Platnumz ambapo kwa sasa msanii huyo ametoka katika Lebo hiyo na kuanzisha Lebo yake ya Konde Gang.

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents