Burudani

Audio: Wizara haina ugomvi na msanii yeyote wa Tanzania – Waziri Shonza

Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) leo tarehe 29 Machi, 2018 akimbatana na Naibu Waziri, Juliana D. Shonza (Mb), Katibu Mtendaji wa BASATA, Mwakilishi wa Bodi ya Filamu Tanzania na Katibu wa Chama cha Muziki wa Kizazi (TUMA) wamekutana na wasanii Roma Mkatoliki na Suzan Michael (Pretty Kind) kujadili maombi yao ya kusamehewa adhabu zao za kufungiwa kujishughulisha kwenye Sanaa kwa kipindi cha miezi 6.

Baada ya majadiliano yaliyochukua zaidi ya masaa 4 Waziri na Naibu Waziri walitoa uamuzi wa kuwafungulia wasanii hao ili waendelee kujishughilisha na kazi za sanaa. Aidha, Msanii Roma alitangaza kuufuta wimbo wake wa “kibamia” na kuomba vyombo vyote vya matagazo nchini kutourusha wimbo huo, ili usiendelee kuleta ukakakasi nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents