Burudani

Roma Mkatoliki akataza media kupiga wimbo wake wa Kiba100 (+Audio)

Baada ya kufutiwa adhabu yake ya kutojihusisha na muziki kwa miezi sita, rapa Roma Mkatoliki amesema ameviomba vyombo vya habari kuacha mara moja kupiga wimbo wake wa Kiba100.

Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari leo Machi 29, 2018. Roma amesema kuwa yeye ndiye mwenye bidhaa hiyo na kutokana na vikao alivyokaa na Waziri Mwakyembe, amejitathmini na ameamua wimbo huo kuufuta kabisa.

Wimbo huo wa Kiba100 ni moja ya nyimbo 15 zilizofungiwa na serikali kupitia BASATA mwanzoni mwa mwezi Machi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents