Michezo

Azam v Toto: Vita yenye tafsri mbili tofauti

Zimesalia saa Chache kabla ya kikosi cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, hakijashuka dimbani kuvaana na Toto African ya mkoani Mwanza, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaokuwa na vita kuu mbili baina ya timu hizo.


Kikosi cha timu ya Azam Fc kikiwa katika mazoezi

Vita hii ni ile ya Azam FC ambayo itakuwa ikisaka pointi tatu muhimu kwa ajili ya kujikita katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, huku ile ya pili ikiwa ni ya Toto ambayo inasaka ushindi ili kujinasua kwenye janga la kushuka daraja.

Azam FC ipo katika nafasi hiyo baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 49 ikiizidi Kagera Sugar inayoifukuzia kwa karibu ikiwa nazo 47, Toto inayowania nafasi ya kubaki Ligi Kuu ipo kwenye nafasi tatu za mkiani (14) baada ya kujikusanyia pointi 29 na inatakiwa kushinda mechi zote mbili zilizobakia ili kujinasua katika mtego huo.

Kikosi cha Azam FC kwa wiki yote hii imekuwa kwenye maandalizi makali chini ya Kocha Mkuu Aristica Cioaba, licha ya mvua zinazoendelea kunyesha kwenye maeneo mengi nchini, yote hayo ni kuhakikisha inashinda mechi zote mbili ilizobakiza na kumaliza ligi katika nafasi tatu za juu.


Kikosi cha timu ya Toto Africans ya Mwanza

Kuelekea mchezo huo, mtaalamu huyo Cioaba amesema kuwa kikosi chake kipo vizuri na wachezaji wake wapo tayari kwa mapambano ya kuwania pointi tatu muhimu, huku akiwaomba mashabiki wa Azam FC kujitokeza kwa wingi kuiunga mkoano timu hiyo kwa kuishangilia.

Cioaba, hakusita kuweka wazi kuwa atawakosa wachezaji wake watatu muhimu kwenye eneo la kiungo, nahodha msaidizi Himid Mao ‘Ninja’, ambaye bado hajarejea nchini baada ya kuwa kwenye majaribio katika timu ya Randers ya nchini Denmark, Frank Domayo, anayesumbuliwa na maumivu ya nyama za nyuma ya paja.

Aidha kiungo Stephan Kingue, naye atakosekana kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano baada ya kupata kadi ya tatu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mbao, ulioisha kwa Azam FC kuichakaza timu hiyo kwa mabao 3-1.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents