Michezo
Azam yashinda tenda ya kuonesha ligi kuu, kumwaga bilioni 23
Kampuni ya Azam Media Limited imeingia makubaliano na shirikisho la soka Tanzania (TFF) ya kuendelea kudhamini ligi kuu Tanzania Bara kwa miaka mitano kwa shilingi bilioni 23.
Hafla ya kuongeza udhamini huo imefanyika jijini Dar es Salaam ambapo kwa upande wa TFF iliwakilishwa na katibu mkuu Selestine Mwesigwa huku kampuni ya Azam ikiwakilishwa na Naibu Mkurugenzi wake Tido Mhando
Kupitia Instagram wa Azam wameandika:
Azam Media Ltd yashinda Tenda ya Kuonyesha Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara nyingine tena, udhamini mnono na wa Kihistoria Bilioni 23