DStv Inogilee!

Baada ya Ghana, Monalisa apata tuzo nyingine Marekani

Msanii wa Filamu Bongo, Monalisa amekabidhiwa tuzo nchini Marekani alipokwenda katika Tamasha la filamu, The African Film Festival (TAFF).

Muigizaji huyo alienda kama host wa tamasha hilo lakini akapatiwa tuzo hiyo kitu ambacho hakukifahamu hapo awali. Kupitia ukura wake wa Instagram Monalisa ameandika;

“Namshukuru Mungu sana kwa anayonitendea, sikujua lolote kuhusu Tuzo, nilialikwa kama Host wa usiku wa Tuzo na kushiriki Tamasha la Filamu. Kumbe TAFF walikuwa wana nia ya kunizawadia Tuzo hii Wow!,” ameeleza.

“Sijui niseme nini mtoto wa Natasha Mimi?watu wa nje wananielewa kiasi hiki kwa kitu ninachofanya kwa ajili ya nchi yangu?ni hisia ambazo siwezi kuelezea,” amesisitiza Monaliza.

Utakumbuka April 14, 2016 Monalisa alishinda tuzo ya The African Prestigious Awards (APA) 2017 kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Kike barani Afrika. Tuzo hizo zilitolewa Accra nchini Ghana, Msani mwingine wa Tanzania aliyeshinda katika tuzo hizo ni Ray Kigosi.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW