Burudani

Baada ya ’Upo Hapo’, Mwana FA, AY & Fid Q ni kundi?, pata jibu

Baada ya Mwana FA, AY na Fid Q kuachia ngoma yao mpya ’Upo Hapo?’, wameeleza iwapo wameunda kundi lao.

Rapper Mwana FA ambaye amechana vilivyo katika verse ya kwanza ya ngoma hiyo amesema umoja huo hauwezi kutengeneza kundi la watu watatu kwani patachimbika.

“Hili haliwezi kuwa kundi kama ulivyoona video ilivyoisha watu wamebadilikiana mwishoni, haiwezi kuwa kundi kila mtu mbabe, kuwa kundi labda kwa dua zenu lakini sisi kama sisi sioni kundi” Fid Q ameiambia Bongo5

Upo Hapo? ni ngoma ya kwanza kuwakutanishwa wasanii hawa watatu kwa wakati mmoja, hapo awali Mwana FA alikutana na Fid Q katika remix ya ngoma ya Nako 2 Nako Soldiers ‘Mchizi Wangu’, wakati AY amekutana na Fid Q katika ngoma kama vile Jipe Shavu, Ujio wa Verse Moja na Shimo Limetema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents