Baada ya Vanessa Mdee, Reekado Banks kuibuka na Harmonize

Kwa inavyooneka huu ni mwaka wa Harmonize kuendelea kuzikamata headlines kwa kufanya kolabo za wasanii wakubwa wa Afrika.

Guess what, kwa sasa Harmonize ameoneka location aki-shoot video na msanii Reekado Banks kutoka Nigeria.

Hivi karibuni Harmonize alikuwa katika media tour nchini Nigeria kabla ya kueleka Ghana na Congo. Bila shaka hayo pia ni matunda ya tour yake hiyo pia.

Utakumbuka Reekado Banks ambaye anafanya kazi na label ya Mavin alishatoa wimbo na Vanessa Mdee uitwao Move uliotoka May 10, 2017.

February 2017 wakati Vanessa Mdee alienda kuitambulisha albamu yake, Money Mondays nchini Nigeria, alisema wimbo huo alioshirikishwa na Reekado Banks ni moja ya nyimbo zinazochezwa sana katika club nchini humo.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW