Habari

Bajeti kufuta jasho wananchi

Mustafa_Mkulo

 

Waziri wa fedha Mustafa  Mkulo, ametangaza bajeti ya fedha sh Bilioni 13,525.9 kwa mwaka 2011 -2012 katika  bunge la Jamuhuri ya muungano Tanzania Dodoma. Watu wengi wameisifu bajeti hiyo, sasa kutokana na unafuu  kwa kunguza  ghalama za baadhi ya vitu vinavyowahusu

 

 wananchi moja kwamoja  na kupandisha baadhi ya vitu ambavyo vimeonekana si vya lazima sana.  Aliliambia Bunge kwamba vitu ambavyo vitakuwa juu, ni vinyaji baridi,bia Sigara,,vinywaji vikali, tumbaku na faini kwa makosa ya usalama  barabarani.

 

Ila pia Mkulo amepunguza kodi ya ongezeko la thamani (VAT), Serikali imesamehe VAT kwenye vipuli vya zana za kilimo, chakula cha kuku, nyuzi zinazotumika kutengenezea nyavu za kuvulia, na mashine za kutifulia udongo, kunyunyizia dawa na kupandia nafaka.

 

Aidha alisema pia wanarejesha kodi za ndani kwa wafanya biashara wadogowadogo kwa bidhaa za ndani ambazo wanauziwa raia wanaosafairi nje ya nchi wataanzia kwenye viwanja vya ndege.  Na nyingine amesema itaondoa nafuu ya VAT, kwa waliopanga nyumba za  shirika la nyumba (NHC), na pia itatoa  nafuu ya VAT katika makampuni binafsi,  kwa vifaa vya matumizi  binafsi kama vile Chakula mavazi na Sabuni, mahsusi kwa watoto yatima na shule.

 

Pia amesema Serikali itasamehe VAT, katika kodi ya  mapato kwenye posho wanazolipwa wafanyakazi wa serikali wanao fanya kazi kwenye taasisi zinazopata ruzuku kutoka kwenye bajeti ya Serikali.

 

Mkulo pia ametia msisistizo kwenye malipo ya mafao wa watumishi wastaafu, pamoja na pensheni zao za kila mwezi.  Pia Serikali itasitisha, ununuzi wa magari ya aina yoyote, labda iwe na sababu maalum tena kwa kibali cha ofisi ya Wazili Mkuu, na vitu vya samani vya ofosini hususani vile vinavyotoka nje.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents