Habari

Balotelli: Ukiona mtu mzima analia……….

Mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli jana amejikuta akilia kama mtoto mdogo baada ya Spain kuifanya kitu mbaya Italia.
Mbaya zaidi baada ya Spain kuinyuka Italia bao 4 kwa ‘nunge’ na kunyakua kombe la Euro 2012, Balotelli alijikuta akikwaruzana na members wengine wa timu yake ya taifa ya Italia.
Baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa mjini Kiev na kuashiria kuwa Italia hawana chao, mshambuliaji huyo wa Manchester City ya Uingereza alijikuta akibishana na viongozi wa juu wa timu hiyo kwenye chumba cha kubadilishia nguo na inasemekana alimsukuma mmoja.
Baada ya dakika kadhaa, Balotelli alionekana tena uwanjani kwenda kupokea medali yake lakini alijikuta akitokwa na machozi ya uchungu na kushindwa kujizuia na hali hiyo.
Hata hivyo kocha wa Italia, Cesare Prandelli amesema Balotelli ataizoea tu hali hiyo iliyomuumiza sana.
‘Niimwambia Mario kwamba haya ni mambo ambayo inabidi ukabiliane nayo na uyakubali,” alisema Prandelli. ‘Inabidi mshikane mkono na uwaambie wapinzani wako kuwa ni wazuri, kubali kushindwa.”
‘Lakini inabidi kuhakikisha kuwa hili linakusaidia kusonga mbele na kukua kutokana na matokeo hayo. Hili limetokea kwa wachezaji wengi, na litatokea tena, lakini hivi ndivyo mchezo ulivyo.’

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents