BurudaniUncategorized

Banky W na mkewe Adesua Etomi wahamishia furaha yao SA

Sherehe za kufurahia ndoa ya Oluwabankole Wellington maarufu kama Banky W na mkewe Adesua Etomi bado zinaendelea.

Wawili hao wameamua kuhamishia furaha yao kwa kupaa na ndege mpaka nchini Afrika Kusini katika mji wa Cape Town kwa ajili ya kumalizia sherehe yao ya tatu ya ndoa ambayo wameipanga kuifanya huko.

Bosi huyo wa kampuni ya Empire Mates Entertainment amefunguka hilo kupitia mtandao wa Instagram kwa kuandika, “Thank you soooo much to all our friends, family and well wishers worldwide. Yesterday was amaaaazing and so much fun my GASH. Now off to Cape town for the finale of our celebration. Love you guyssss.”

Banky na Adesua walifunga ndoa yao ya kimila siku ya Jumapili iliyopita na jana (Jumatatu) walifanikiwa kusaini hati za kisheria ndoa yao kutambulika na serikali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents