Barakah The Prince aweka wazi sababu ya bifu lake na Nay Wamitego (Audio)

Unaifahamu sababu ya Nay Wamitego kumchana Barakah The Prince kwenye wimbo wa ‘Moto’ ambao aliuachia Juni mwaka jana?

Barakah ameweka wazi sababu ya kuchanwa kwenye ngoma hiyo. Msanii huyo amesema sababu alimwambia Nay kuwa kipaji chake ni kidogo na hawezi kurap.

“Nilitoka studio nikamkuta [Nay] anadiss kuhusu Godzilla, mimi nikamwangalia nikamwambia huyu jamaa mbona kipaji chake kidogo sana?,” Barakah amemuambia mtangazaji wa Jembe FM, JJ.

“Ujue Godzilla ni rapper sasa wewe Nay Wamitego unarap kitu gani? Haumfikii Godzilla hata kidogo, wewe ni msanii unaunga unga. Hapo ndipo alipopaniki akaamua kwenda kuniimba, siwezi kumjibu mtu ambaye hana kipaji,” ameongeza.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW