Michezo

Barnaba atoa tahadhari kwa wasanii wa kike “Hamisa Mobetto anakuja kuwanyang’anya kijiti”

Barnaba atoa tahadhari kwa wasanii wa kike "Hamisa Mobetto anakuja kuwanyang'anya kijiti"

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Barnaba amefunguka na kutoa ya moyoni kwa kuwaasa wasanii wa kike wa muziki wa kizazi kipya alimaarufu Bongo Fleva kuhusu uwajibikaji wao katika muziki wahofie kupokonywa kijiti na msanii mwenzao ambaye anafanya vizuri na kibao chake kipya cha ‘Tunaendana’ mwanadada Hamisa Mobetto.

akiongea hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram barnaba amefunguka hayo kwa kutoa maoni yake chini ya post ya Hamisa ambayo alipost nyimbo yake hii mpya na Barnaba kuandika kuwa:-

” Yani hala hala sana kabisa hii sauti kila hatua na sekunde zinavyozidi kugonga ndo inazidi kukomaa,narudia tena hala hala sana kwa walioshikilia vijiti wawezapokonywa vijiti”


Hamisa Mobetto ameachia video ya wimbo wake wa ‘Tunaendana’ ikiwa ni wimbo wake wa pili baada ya wimbo wa Madame hero kufanya vizuri na kufanikiwa kupata nafasi ya kufanya show nje ya nchi hasa nchini Marekani.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents