Michezo

Barua ya Malinzi kwa wajumbe Mkutano Mkuu TFF

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi anayemaliza muda wake, ameishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli, wadhamini mbalimbali, washirika na wadau wa soka kwa ushirikiano walioutoa katika kipindi chote cha uongozi wake.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi

Taarifa ya Malinzi kupitia kwa mawakili wake, Kampuni ya Rwegoshora leo imesema kwamba ana imani viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi wa Agosti 12 mjini Dodoma watatilia mkazo mambo muhimu katika soka la Tanzania, ikiwemo soka la vijana na wanawake, maandalizi ya Fainali za vijana ya umri wa miaka 17 Afrika mwaka 2019 na kuboresha miundombinu ya mchezo kwa ujumla.

Malinzi amewatakia Wajumbe wa Mkutano Mkuu na wagombea wote uchaguzi mwema utakaofungua ukurasa mpya katika soka ya Tanzania.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents