Soka saa 24!

Barua ya wazi kwa Darassa: How you can capitalize on your music success

Dear Darassa,

Kwanza kabisa ningependa nichukue nafasi hii kukupongeza kwa mafanikio makubwa ya single yako ya Muziki, kiukweli ni nyimbo ambayo kwa mwaka 2016 imekuwa gumzo na japokuwa sina data za kutosha naweza thubutu kusema inaweza kuwa ni ndio nyimbo iliyosikilizwa zaidi na kuwafikia watu wengi sana kwa muda mfupi toka ilipotoka.

Lengo kubwa la mimi kukuandikia “open letter” hii ni kujaribu kuelezea ideas zangu ambazo nahisi zinaweza kukupa “support” zaidi kwenye safari yako ya kuwa mmoja wa wasanii wakubwa ndani na nje ya nchi yetu hasa ikizingatiwa ya kwamba muziki wetu upo kwenye “direction” nzuri sana ya kuwa mkubwa zaidi barani Afrika.

Pili, haya ni mambo ambayo nimekuwa nikiyawaza kwa muda mrefu zaidi juu wa wasanii wa muziki wa hapa Bongo na kuyatafakari kwanini hayafanyiwi kazi na wadau wa muziki au hata kama yanafanyiwa kazi mbona “impact” yake hatuioni kivile?

Disclaimer: Naandika haya mambo kama mawazo tu kutokana na experience yangu ya biashara zangu na pia kupitia experience ya kuangalia watu wengine wanafanyeje. “I’m not claiming to be an expert” kwenye music or kwenye biashara. Kuna uwezekano mkubwa vitu nitakavyosema hapa visiwe applicable kwako kutokana sababu zako binafsi au plans zako za kimuziki. Na wala sitoi guarantee yoyote kuwa mambo haya yatafanya kazi kama ninavyosema. “They are just ideas that you can choose to work on them or trash them”

Tukiachana na ‘disclaimer’ hapo juu, vitu vitatu tu ambavyo ningependa kuvielezea leo ni
1. Branding
2. Monetization strategies
3. Self-promotion

1. Branding

Kwanza kabla ya kuelezea kuhusu branding naomba niseme kuwa kaka mkubwa umetoboa. You are a star now, maana sio kwa attention na positive response ambayo Muziki imepata. Kutoka kwako nakufananisha na kipindi ambapo Wiz Khalifa wakati anaanza muziki. Alitoa track chache ambazo zilisikika sikika kisela then baadaye akatoa “Teach U to Fly” na “Say yeah” ambazo zilifanya vizuri zaidi kabla ya kutoa “Black and Yellow” ambayo ilibadilisha kila kitu kwake.

Tofauti na sisi wabongo mbele watu sababu wanajua muziki zaidi na wanajua biashara, once wakitoa kitu kikakubalika na jamii huwa ‘immediately’ wanajua nini cha kufanya ili kuji-brand kama wasanii wakubwa kuendana na soko. Na branding nayoingelea hapa sio branding ya lifestyle na mavazi au level za bata, ni branding ya kuji – associate wewe na muziki wako kwamba watu wajue Darassa ni nani, na ndo yule aliyeimba ule wimbo wa muziki hata wakiamshwa usiku wa manane.

Maana nachokiona ni kwamba wimbo huu umekuwa mkubwa sana, lakini nachojiuliza ni, Je? Jina lako linakuwa sambamba na wimbo? Watu wanakujua Darassa kama Darassa? Na kila wakiusikiliza / kuutazama wimbo YouTube wanakumbuka jina la mwanamuziki nyuma yake?

Hii ishu niliiwaza sana pia wakati Man Fongo katoa wimbo wake wa ‘Hainaga Ushemeji’, maana ule wimbo kwakweli kama ni kutusua Man Fongo alitusua ila Je, watu wamemjua Man Fongo kama Man Fongo? Au wamebaki kukumbuka tu phrase ya “hainaga ushemeji” na kumsahau Man Fongo? Na vipi kesho akitoa/ukitoa wimbo mwingine watu watalikumbuka jina lako hata kama wimbo sio mkali kama huu na hauna a catchy phrase kali kama “hainaga ushemeji” au “acha maneno weka mziki”?

Moja ya case study yangu nzuri sana ya hii type ya branding ni kwa kuangalia na kujifunza nini Soulja Boy alikifanya alipotoboa na wimbo wake wa “Crank That” mwaka 2007 au juzi hapa Desiigner alipotoa Panda au T-pain alipotoboa na matumizi yake ya autotune kwenye nyimbo.

Ni kweli hatuwezi kujilinganisha na “resources” walizonazo wenzetu lakini tunaweza kujifunza kutoa kwao. Ingawa crank dance zilikuwepo before, Soulja Boy aliweza kuji-brand na crank kiasi kwamba mpaka leo mtu akiwaza crank dance lazima amkumbe Soulja Boy kwa njia moja ama nyingine, the same applies to T-Pain na auto-tune au “Panda” na “Desiigner”

2. Monetization strategies

Najua bado ni changamoto hapa nchini kwa wasanii kunufaika moja kwa moja kupitia single zao wanazotoa kwa njia mbadala tofauti na show na caller tunes ambazo wengi wenu ndo mmeanza kunufaika siku za karibuni. Lakini pamoja na chagamoto hizi bado mi naona bado kuna opportunities nyingi sana ambazo wasanii wanaweza kuzitumia ili wanufaikezaidi na singles zao na kuacha kutugemea shows tu.

Mfano, kupitia hii nyimbo yako ya Muziki, baadhi ya vitu ambavyo management yako ingewezza kuvifanya ili wewe ufaidike zaidi ni pamoja na hivi vifuatavyo:

1. Public Sponsored shows

Hizi ni shows ambazo management yako inaweza kuzindaa kwa ajili ya public lakini zikadhaminiwa na makampuni machache. Tofauti na ilivyo sasa ambako makampuni ndo yanandaa show na kukuita wewe, unaweza ukaandaa wewe show na kuyafuta makampuni kuyaambia kuwa utatangaza bidhaa zao kwenye show yako kwa gharama fulani ambayo sio kubwa na wenyewe wanaweza kuja kuuza/kutangaza bidhaa zao hapo maana mkusanyiko utakuwepo maana ni uhakika watu wakakuja kusikiliza muziki.

Ukipata hata kampuni 10 zikakupa milioni 2 -3 ukafanya hii routine kwa mikoa mitano mikubwa, nadhani kuna number zitaongezeka benki a pia itakusaidia kukuza jina lako kwa mashabiki.
Na sio lazima utafute makampuni makubwa kama Tigo au Vodacom, zipo mid-sized companies ambazo zinazoweza kutoa hela hiyo bila shida yoyote au a long procedure itakayokufanya ushindwe ku-execute plan yako on time.

2. Mauzo ya branded Tshirts/kofia

Hili lipo wazi nadhani na naona kuna wasanii wanafanya tayari. Kuprint t-shirt na kofia sio kazi, tena unaweza ukaagiza mzigo fasta tu China ukaja ndani ya wiki. Uzuri kwa wewe wimbo wako una catch phrase safi kabisa “Acha maneno, weka muziki” . I’m sure watu kibao watachangamkia t-shirt zako na kofia ambazo unaweza kuzioua kupitia kwenye shows zako hizo za wazi au hata kupitia mtandao

3. Mauzo ya branded accessories

Hii pia ni kama mauzo ya t-shirts na kofia tu. Unaweza print vitu kama car stickers, stickers za boda boda, bajaji na ntingine kibao tu watu wazinunue na ukauza kwa staili kama ya Tshirts au kofia

4. Youtube Video

Nimekuwa nikifuatilia channel yako ya Youtube na sioni kama unaitumia effective kukuingiiza kipato cha ziada. Angaliana jifunze kupitia channel ya Diamond au wasanii wengine huko mbele. Vitu kama behind the scenes, interviews, funny clips zako, studio sessions, tours n.k vinaweza kuwa opportunity ya wewe kutengeneza passive income nzuri tu. There is a reason why wasanii wakubwa wa nje wanakuwa na personal videographer wao au ptotographer na wanapost post vitu Youtube. Sio kwa ajili ya fans tu. Kuna hela pia nzuri sana ya kutengeneza hapo

5. Online Store /website

Unaweza kuset up online store au website yako ambayo watu wanaweza kununua vitu vilivyotajwa hapo juu kwa urahisi zaidi na pia inakuwa ni njia moja ya ku-control wa mauzo yako halisi na fake toka kwa watu wanao duplicate kazi zako. Yote haya na mambo mengine mengi ambayo sijayataja ni mambo ambayo management yako inaweza kujipanga na kuyafanyia kazi (kama haijaanza kuyafanyia kazi sasa hivi) taratibu kuanzia kwenye wimbo huu wa muziki na nyimbo zake nyingine zinazokuja

3. Self-Promotion

Kitu cha tatu na cha mwisho ambacho ningependa kuki-adress ni self-promotion.
Nimejaribu kupitia social media accounts zako kuangalia nini unafanya na naona bado sula la self-promotion yako inabidi uli-upgrade kidogo kama inawezekana.

Facebook : page likes – 315 tu
Twitter : followers 952 tu
Instagram : folowers 818 tu
Youtube : 22,842

Kwa muda huu ambapo Muziki ndo habari ya mjini hizi number zingetakiwa ziwe zinakuwa sawa na idadi ya watu wanaosikiliza muziki, maana hawa fans ndo listeners/viewers wa ngoma yako ya kesho. Wakiwa wengi zaidi ndo track yako inavyosambaa kwa haraka zaidi na kuwafikia watu wengi zaidi. Kama unazi-manage mwenyewe hizi accounts tafuta hata dogo basi wa kuzi-keep busy on the side ukiwa wewe una mambo mengine ya kufanya. I’m sure huwezi shindwa ku-afford kumlipa hata elfu 50 kwa wiki.

Angalia mfano wa social media accounts za kina Chris brown kuanzia Facebook mpaka Instagram utaona jinsi wenzetu wapo serious na self-promotion. Na hili sio kwako tuu, nimekuwa nikiangalia accounts za wasanii kibao hapa bongo wengi social media zao ni majungu tu na vijembe badala ya kutumia kama platform za kuwaingizia kipato.

Ukitazama wenzetu especially kwenye situation kama hizi wanapokuwa kwenye chat utafurahi jinsi walivyo serious na self-promotion. Kuna vitu vidogo unaweza fanya ilikuwa- incentives mashabiki waondelee kuiongelea ngoma yako zaidi. Mfano mwingine mzuri ni Tekno miles alipotoa track yake ya“Pana”, kama ulimfuatilia kidogo nadhani uli-notice jinsi gani alivyokuwa serious ku-promote ngoma yake mpya hiyo maana alijua ni hit song na inahitaji kupushiwa zaidi.

Conclusion

Kama nilivyosema hapo awali, lengo langu ni kujaribu kuweka wazi mawazo yangu ambayo naamini yanaweza kuwa ni changamoto kwako na kwa wasanii wengine watakaoweza kupata nafasi ya kutoboa kama wewe. Nachokiamini mwisho wa siku muziki huu unaoufanya lazima ukulipe kwa namna moja au nyingine ndo maana umekomaa miaka yoye hii kufika hapo ulipo. Na mimi kama mtanzania mwenye kujivunia kazi nzuri za watanzania wenzangu sina budi ku-support kizuri kutoka nyumbani.

Inawezekana niliyoyasema hapo tayari mnayafanyia kazi au yapo kwenye pipeline ila all in all I had to say something maana Muziki imekuwa ni ngoma kubwa sana na nimefurahi pia maana imezinyamazisha zile pande kubwa mbili zenye maneno mengi sana mtandaoni na sasa hivi wamenyamaza wanaweka muziki tu.

I wish you get the best in your career and I wish utoe ngoma kali zaidi ya muziki.

Acha maneno, weka muziki

By TZ Anonymous

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW