Michezo

Francis Cheka atangaza ramsi kustaafu ngumi

Bondia Francis Cheka ametangaza rasmi kuachana na mchezo wa ngumi na kujielekeza kwenye masuala binafsi ya kibiashara.

Mwanandondi huyo kutoka Morogoro amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari wa ITV mjini Morogoro kuhusu taarifa zilizoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari na kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii vikimhusiha na utapeli wa kukimbia ulingoni Dec 25 mwaka huu huko jijini Dar es Salaam, alikotakiwa kupigana na bondia Dula Mbabe,ambapo amebainisha kutofika ulingoni siku hiyo hakukumaanisha kuhofia pambano hilo bali ni kutokana na promota wake Kaike Selagi kutomlipa fedha zake zote kama walivyokubaliana, ambapo amedai alipaswa kulipwa milioni tisa, lakini hadi wanamaliza kupima uzito alikua amepewa milioni tatu pekee.

Akizungumzia azma ya kuachana na ngumi,Cheka amesema kwa muda mrefu amekuwa akipigana bila mafanikio kutokana na kudhulumiwa na waandaaji au kulipwa tofauti na makubaliano sambamba na misukosuko ya hapa na pale anayofanyiwa na wapinzani wake na kwamba anaamini wapo baadhi ya watu waliolenga kumshusha kwenye ngumi badala ya kumtengeneza bondia mwingine mwenye uwezo na kumpiga na kwamba kwa sasa atajielekeza kufanya biashara zake na kuahidi ushirikiano kwenye mchezo wa ngumi ili kukuza na kuendeleza mchezo huo.

Source: ITV

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents