Burudani ya Michezo Live

Bashe, Simbachawene wateuliwa na Rais Magufuli, January Makamba adai “Nitasema zaidi siku zijazo”

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Magufuli amemteua Hussein Mohamed Bashe, kuwa Naibu Waziri wa Kilimo. Bashe anachukua nafasi iliyoachwa na Mh. Innocent Bashungwa ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

Rais Magufuli pia amemteua George Boniface Simbachawene, kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, akichukua nafasi ya January Makamba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Kufuatia uteuzi huo, January Makamba amesema ameupokea kwa mikono miwili na kuahidi kuwa ataongea mengi zaidi baadae.

“Kwa kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa kabisa 😊. Nitasema zaidi siku zijazo.” ameandika Makamba kwenye ukurasaa wake wa Twitter.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW