Michezo
Bastian Schweinsteiger ataendelea kuwa nje ya uwanja kwa mwezi mzima
Mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani na Kiungo wa klabu ya Man United ya Uingereza Bastian Schweinsteiger January 31 imetoka taarifa sio njema kuhusu yeye.
Sport1 wametoa taarifa za kuwa Schweinsteiger mwenye umri wa miaka 31 ataendelea kuwa nje ya uwanja kwa mwezi mzima, Schweinsteiger anauguza goti la kulia la mguu wake.