Burudani

BBA: Davido (Nigeria) kuperform leo kwenye Eviction Show


Mwanamuziki chipukizi aliyejipatia mafaniko makubwa nchini Nigeria, David Adeleke maarufu kwa jina la Davido kesho atapanda kwenye stage ya Big Brother Africa Stargame kwenye show ya Eviction usiku huu.
Davido ni msanii na producer aliyeanza muziki mwaka mmoja tu uliopita.
Staa huyo ameanza kuimba tangu akiwa na miaka 11, na kwa muda mfupi mno amejipatia mashabiki lukiki nchini Nigeria, Marekani, Uingereza na kote barani Afrika.
Wimbo wa mwanamuziki huyo mwenye umri mdogo uitwao “Dami Duro unapewa nafasi ya kuwa club banger na kupokea airplay ya kutosha barani Afrika.
Mpaka sasa Davido ameshapanda stage moja na wasanii wakubwa kama Fabulous, Keith Sweat, Cabo Snoop, D’banj, Naeto C na wengine.
Mwanamuziki huyo pia anatarajia kuzindua albam yake ‘Omo Baba Olowo’ (OBO), July 22, jijini Lagos.
Davido ambaye ni mtoto wa billionaire wa nchini Nigeria, Deji Adeleke, mwenyekiti wa kampuni ya Keplo-Pacific Energy Pacific inayoshughulika na mambo benki, vyuma na umeme, amesainishwa kwenye label ya D’Banj, DKM Records.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents